Sasa ni afueni kwa waziri mteule wa utalii Peninah Malonza baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha majina yote ya mawaziri wateule ikiwemo la Bi. Malonza. Malonza alinusuriwa baada ya bunge kukataa pendekezo la kamati hiyo kuwa asiidhinishwe. Wabunge wa mrengo wa Kenya Kwanza, waliunga mkono kuidhinishwa kwa Malonza, wakisema ana tajiriba ya kutosha na anapaswa kupewa fursa ya kuhudumu. Sasa majina ya mawaziri wateule walioidhinishwa yatawasilishwa kwa rais kwa uteuzi rasmi.
Pwani Media Network ( K) is an online news hub that focuses on human interest stories around the Coastal region. Our aim is to satisfy you and keep you updated on what's happening in and outside the region. Pwani Media Network "News At Your Finger Tips" Want coverage? email to pmwarandu82@gmail.com