Na
Mwarandu Randu
Jamii ya watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Mombasa wamepinga hatua ya kuwatathmini inayotekelezwa kila baada ya miaka mitano na baraza la kitaifa la walemavu, National Council for People Living with Disability (NCPWD).
Kushoto, mkurugenzi mkuu wa Tunaweza Women with Disability Charity Chahasi na Lucy Chesi (picha) na Mwarandu Randu |
Jamii ya watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Mombasa wamepinga hatua ya kuwatathmini inayotekelezwa kila baada ya miaka mitano na baraza la kitaifa la walemavu, National Council for People Living with Disability (NCPWD).
Akiongea na wanahabari Lucy Chesi kutoka bunge la walemavu kaunti ya Mombasa ametaja hatua
hiyo kama dhulma dhidi ya walemavu.
Amesistiza kuwa ni sharti baraza hilo liwatathmini walemavu
kote nchini mara moja tu na wala sio kila baada ya miaka mitano.
Chesi aidha amesistiza kuwa wameanzisha miradi ya kuwawezesha walemavu ili wapate kujinufaisha kiuchumi.
Wakati huo huo, Charity
Chahasi mkurugenzi wa shirika la kijamii la Tunaweza Women with Disabilty lililoko Ziwa la Ng'ombe amelitaka baraza
la walemavu nchini kuheshimu haki za
walemavu kwa kuzingatia mfumo wa sheria nchini.
Amelishtumu vikali baraza hilo kwa kile anachodai ni kukiuka haki za walemavu sawia na kuwadhulumu walemavu nchini.
Hata hivyo amesema kuna haja ya baraza hilo kutafuta
njia mbadala ya kuwatathmini walemavu ikiwemo kuwapa vitambulisho vya kudumu
wala sio baada ya miaka mitano.
Wamewataka walemavu kaunti ya Mombasa kujitokeza kwa wingi ili kupigania haki zao katika jamii.
Comments
Post a Comment