Na
Mwarandu Randu
Jamii
ya watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Mombasa wanaitaka serikali ya kaunti ya kufuata
mpangilio maalum wa ukarabati wa barabara na maeneo ya umma sawia na kujenga vivukio maalum kwa walemavu.
Walemavu hao wanadai kuwa ukarabati unaotekelezwa
katika maeneo mengi ya mji hauzingatii matakwa ya walemavu hao.
Mkalla
Shanga mmoja wa walemavu hao amesema walemavu wanalipa
ushuru kama wakenya wengine hivyo wana haki ya kupata huduma bora katika maeneo
ya umma.
Amesistiza kuwa ni jukumu la serikali ya kaunti kujenga
maeneo maalum kwa walemavu ili kurahisishha matembezi yao jijini.
Wakati uo huo, Charity
Chahasi mmoja wa walemavu hao amesema kulingana na katiba ya mwaka 2010 sehemu
zote za umma zinastahili kuangazia masuala ya walemavu.
Amesema walemavu wana haki ya kupata huduma bora katika maeneo ya umma.
Anadai kuwa ukarabati wa mji unaoendelea katika
kaunti ya Mombasa haujatilia maani jamii ya walemavu.
Hata hivyo ameitaka serikali ya kaunti kungazia kwa
makini swala hilo ili walemavu warahisishiwe matembezi yao mjini.
Comments
Post a Comment