Wahudumu wa afya wakujitolea waitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuweka mikakati ya kuwalipa mishahara ya kudumu
Na
Mwarandu Randu
Mhudumu wa afya mashinani akitoa huduma kwa wanajamii FILE PHOTO |
Wahudumu
wa afya wa kujitolea kutoka nyanjani wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuweka
mikakati thabiti ili waweze kupata mishahara ya kudumu.
Akizungumza na wanahabari kaunti ya Mombasa Jennifer Muthoni mmoja wa wahudumu hao kutoka
Mikindani amesema wanapitia
changamoto si haba wakati wanapowahudumia wanajamii.
Amesisitiza kuwa malipo hayo yataweza kukidhi baadhi
ya mahitaji ya jamii zao huku akisema kuwa wana kazi ya ziada mashinani.
Vile vile, ameongeza kuwa wahudumu hao ni kiungo
muhimu kwa jamii hasa ikizingatiwa kuwa huwasaidia maafisa wa afya mashinani.
Wakati uo huo,Charity
Baya kutoka eneo bunge la Jomvu amesema
serikali ya kaunti ina jukumu la kuwalipa wahudumu hao kufuatia kazi wanayoitekeleza
mashinani.
Ameongeza kuwa wengi wao wamekosa ajira hivyo hutegemea
sana huduma hiyo.
Charity aidha ameitaka serikali ya kaunti kuangazia
kwa makini suala hilo ili wahudfumu hao waweze kupata mapato yatakayokidhi
mahitaji yao.
Comments
Post a Comment