Na Kombe Peter
Baadhi
ya jamii ya watu wanaoishi na ulemavu wameombwa kukoma kulalamika na badala
yake wajitokeze katika kutafuta nyadhifa za uongozi katika jamii.
Akizungumza na wanahabari kaunti ya Mombasa mkurugenzi
wa shirika la kutetea haki za walemavu la Pamoja
Twaweza Ruth Awinja amesema hulka
ya walemavu ya kualalamika kila mara haiwasaidii kivyovyote.
Amesema kuwa ni jukumu la walemavu hao kuapata elimu ya kutosha kama wakenya
wengine ili kupata nafasi hizo.
Hata hivyo amesistiza kuwa shirika hilo huangazia
masuala yanayoathiri walemavu mashinani.
Kwa upande wake, Mkalla Shanga mmoja wa walemavu hao amesistiza haja ya kuzingatiwa kwa sheria ya kuwateua walemavu
katika nyadifa za uongozi.
Ameongeza kuwa maswala ya walemavu ni haki yao ya
kimsingi hivyo ni sharti yetekelezwe.
Comments
Post a Comment