![]() |
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akisalimiana na hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal. PICHA Mwarandu Randu |
Mwarandu
Randu na Godfrey Aluda
Gavana
wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho na hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal
wameamua kuzika tofauti zao za kisiasa kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa.
Wakizungumza na wanahabari leo katika afisi za gavana
hapa jijini Mombasa, Joho amesema kuwa
tofauti za kisiasa sio kigezo cha kutengana na kuwekeana uadui baina yao.
Joho amedokeza kuwa ataendelea kufanya majadiliano
ya mara kwa mara na mpinzani wake ili kutafuta suluhu la kudumu kwa changamoto zinazowakabili wakaazi
wa Mombasa.
Hata hivyo gavana huyo amepongeza mwafaka wa
maelewano baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga.
Wakati uo huo, Suleiman
Shahbal amewataka viongozi wa ukanda wa pwani kuzika tofauti zao za kisiasa
na badala yake waangazie miradi ya maendeleo.
Shahbal hata hivyo ameitaka serikali kuu kuwapa
kipaumbele wawekezaji wa humu nchini wakati wa kutekelezwa kwa mradi wa Dongo Kundu.
Amesema kuna haja ya serikali kuu kuzingatia
kikamilifu wawekezaji wa humu nchini huku akisistiza kuwa wana uwezo wa kuteleleza
mradi huo.
![]() |
Gavana Joho Suleiman Shahbal na Gavana wa Nairobi Mike Sonko |
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi amewahimiza viongozi nchini
kukumbatia mwafaka huo ili kuwanunganisha wananchi mashinani.
Aidha Sonko amewapongeza viongozi hao kwa kukubali
kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuamua kushirikiana katika kukuza uchumi
wa kaunti ya Mombasa.
Itakumbukwa kwamba gavana joho na Suleiman Shahbal
walikuwa mahasimu wa kisiasa katika uchaguzi mkuu uliopita.
Breaking all the bits and bites
ReplyDelete