Katibu katika wizara ya habari mawasiliano na teknolojia Jerome Ochieng ahimiza ushirikiano baina ya serikali na sekta ya kibinafsi
Katibu katika wizara ya habari mawasiliano na teknolojia Jerome Ochieng Picha (Maktaba) |
Na
Godfrey Aluda na Peter Mwarandu
Katibu
katika wizara ya habari, mawasiliano na teknologia Jerome Ochieng ametaka
kuwepo kwa ushirikiano mwema baina ya serikali na sekta ya kibinafsi ili kukuza
na kuendeleza mfumo wa mawasiliano ya kimtandao nchini.
Akizungumza leo hapa jijini Mombasa katibu huyo
amesema serikali inafanya kila jitihada ili kuboresha huduma za mtandao katika
sekta nchini.
Katibu huyo hata hivyo amedokeza kuwa ili kuafikia
malengo hayo serikali kupitia kwa wizara hiyo inanuia kuwekeza zaidi katika
miundo misingi ya mawasiliano na teknolojia.
Ameongeza kuwa wizara hiyo itawekeza zaidi katika
mfumo wa mawasiliano ya nyaya za
baharini ili kurahisisha utenda kazi katika sekta mbali mbali za serikali.
Jerome aidha amesistiza kuwa wizara hiyo
itahakikisha kuwa mradi wa Mama Ngina uliozinduliwa hivi majuzi na rais Uhuru Kenyatta
unaunganishwa na huduma za kimtandao ili kurahisisha mawasiliano eneo hilo.
Comments
Post a Comment