Haki Africa yaitaka idara ya polisi kuchunguza kupigwa kinyama kwa mmoja mtaa wa bombolulu kaunti ya Mombasa
Na Godfrey aluda / Mwarandu Kombe
Mathias Shipeta afisa wa kitengo cha dharura katika shirika la kijamii la HAKI Afrika |
Shirika la kutetea
haki za kibinadamu la Haki Africa limeitaka idara ya usalama kaunti ya Mombasa
kufanya uchunguzi wa kina na kuwatia nguvuni wahudumu wa boda boda
wanaodaiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 28
katika eneo la Bombolulu mapema juma hili.
Kulingana na afisa wa
kitengo cha dharura katika shirika hilo Mathias Shipeta kijana huyo alivamiwa
na baadhi ya wahudumu wa boda boda wanaohudumu eneo hilo ambao walimpiga na
kujeruhi vibaya baada ya kulumbana na mmoja wao.
Akizungumza na
wanahabari mjini Mombasa Shipeta amelaani vikali kitendo hicho na kuitaka
idara ya usalama eneo hilo kuhakikisha kuwa uchunguzi unafanywa .
Shipeta aidha
amefichua kuwa baadhi ya wahalifu hujifanya wahudumu wa boda boda na
kuwaharibia jina wahudumu hao.
Amewataka wahudumu hao
kutoa taarifa kwa maafisa wa polisi ili wahalifu hao wakabiliwe vilivyo.
Kijana huyo anaendelea
kupokea matibabu katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani .
Comments
Post a Comment