Na
Godfrey Aluda / Mwarandu Kombe
Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja picha (Maktaba) |
Gavana
wa Taita Taveta Granton Samboja amewataka viongozi wa kisiasa nchini kutowagawanya
wakenya kwa misingi ya kikabila.
Akizungumza leo hapa jijini Mombasa wakati wa
ufunguzi rasmi wa kongamano la viongozi wa kaunti hiyo gavana huyo amesisitiza
haja ya wanasiasa kuzingatia maendeleo
yatakayowafaa wakenya.
Amesema msimu wa siasa umepita na kilichobaki ni
kuwafanyia kazi wakenya.
Wakati uo huo, Samboja ameunga mkono kuchaguliwa kwa
gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kama mwenyekiti wa baraza la magavana
nchini.
Samboja aidha amedokeza kuwa kuchaguliwa kwa gavana huyo
kulitekelezwa katika njia ya uwazi huru na haki.
Itakumbukwa kuwa hivi majuzi gavana wa kaunti ya
Kwale Salim Mvurya alipinga uchaguzi huo akisema kuwa kulikuwepo mkataba wa
maelewano ili kumrithi aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo Josphat Nanok.
Vile vile gavana huyo amesema baraza la magavana
litahusika kikamilifu katika mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba ili
kugatua fedha zaidi mashinani.
Comments
Post a Comment