Skip to main content

Gavana Joho na hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal wazika tofauti zao za kisiasa



Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akisalimiana na hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal. PICHA Mwarandu Randu
Mwarandu Randu na Godfrey Aluda

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho na hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal wameamua kuzika tofauti zao za kisiasa kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa.

Wakizungumza na wanahabari leo katika afisi za gavana hapa jijini  Mombasa, Joho amesema kuwa tofauti za kisiasa sio kigezo cha kutengana na kuwekeana uadui baina yao.

Joho amedokeza kuwa ataendelea kufanya majadiliano ya mara kwa mara na mpinzani wake ili kutafuta suluhu  la  kudumu kwa changamoto zinazowakabili wakaazi wa Mombasa.

Hata hivyo gavana huyo amepongeza mwafaka wa maelewano baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga.

Wakati uo huo, Suleiman Shahbal amewataka viongozi wa ukanda wa pwani kuzika tofauti zao za kisiasa na badala yake waangazie miradi ya maendeleo.

Shahbal hata hivyo ameitaka serikali kuu kuwapa kipaumbele wawekezaji wa humu nchini wakati wa kutekelezwa kwa mradi wa Dongo Kundu.

Amesema kuna haja ya serikali kuu kuzingatia kikamilifu wawekezaji wa humu nchini huku akisistiza kuwa wana uwezo wa kuteleleza mradi huo.

Gavana Joho Suleiman Shahbal na Gavana wa Nairobi Mike Sonko
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi amewahimiza viongozi nchini kukumbatia mwafaka huo ili kuwanunganisha wananchi mashinani.

Aidha Sonko amewapongeza viongozi hao kwa kukubali kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuamua kushirikiana katika kukuza uchumi wa kaunti ya Mombasa.

Itakumbukwa kwamba gavana joho na Suleiman Shahbal walikuwa mahasimu wa kisiasa katika uchaguzi mkuu uliopita.




Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Involve all stakeholders when proposing new laws- BOTTAX General Secretary petitions government

BOTTAX General Secretary Cynthia Wanyonyi Photo (courtesy) BY PETER KOMBE Kenya Boda Boda Tuk Tuk and Taxi Workers Union (BOTTAX Kenya) has faulted the government on claims of passing bills that do not favor the transport sector. Speaking to the media in Mombasa on Monday the union’s General Secretary Cynthia Wanyonyi said in most cases the government does not involve boda boda Tuk Tuk and other informal transport worker's representatives. She further noted that as stakeholders in the public transport sector the government fails to carry out effective public participation exercises as enshrined in the Kenyan constitution. “The government does not involve the public when making certain decisions,” she noted. Wanyonyi urged both the operators to register with the union to avoid being misled by what she claims are quack organisations. She urged the department concerned with registering cooperatives and other associations touching on the informal trans...

MALONZA AIDHINISHWA

Sasa ni afueni kwa waziri mteule wa utalii Peninah Malonza baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha majina yote ya mawaziri wateule ikiwemo la Bi. Malonza. Malonza alinusuriwa baada ya bunge kukataa pendekezo la kamati hiyo kuwa asiidhinishwe. Wabunge wa mrengo wa Kenya Kwanza, waliunga mkono kuidhinishwa kwa Malonza, wakisema ana tajiriba ya kutosha na anapaswa kupewa fursa ya kuhudumu. Sasa majina ya mawaziri wateule walioidhinishwa yatawasilishwa kwa rais kwa uteuzi rasmi.

Learn instrumentals and write your own songs- Eric Wainaina tells upcoming artistes.

Eric Wainaina delivering a keynote address at Aga Khan Academy Mombasa on Saturday during the academy's 13th graduation ceremony   BY PETER KOMBE Eric Wainaina famed for his “Nchi ya Kitu Kidogo” song has told upcoming artistes to learn musical instruments besides writing their own songs. According to him this is the only way to stay relevant in the industry which he terms as being competitive. He says his new album ‘Dreams in Stereo’ is currently available in all digital platforms including mdundo.com, skiza and amazon tunes. The famed artiste says “the new album is one of my fine works.” The artist however denied claims that he was working behind the curtain rather he says he had earlier on produced two albums which according to him did not get good airplay. “The music industry like any other industry has both ups and downs,” he said. The new album “ Dreams in Stereo” is a vivid description of my life, love, passion and betrayal.” Asked wh...